×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Ili Kulinda Misitu, Tanzania yafikiria kuweka tozo kwenye mkaa

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Monday, 23 January 2017 07:10 GMT

A cyclist transports charcoal for sale at Ngozi village near Malawi's capital Lilongwe, February 2, 2016. REUTERS/Mike Hutchings

Image Caption and Rights Information

Making the fuel more expensive could help cut surging demand, officials believe

DAR ES SALAAM, Tanzania, Jan 23 (Thomson Reuters Foundation) - Tanzania inakusudia kuweka tozo kwenye mkaa kwa lengo la kuzuia matumizi ya nishati hiyo ambayo ni chanzo kikubwa cha nishati ya kupikia lakini pia inachangia pakubwa katika uharibifu wa misitu.

Maofisa wanasema wanaamini kufanya mkaa bei ghali zaidi utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi yake na ukataji holela wa miti kwenye taifa hilo la Africa Mashariki.

Justus Ntalikwa, Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini aliiambia Thomson Reuters Foundation kwamba serikali inakusudia kuwasilisha muswada bungeni Mwezi February kuweka tozo hiyo, na pesa zitakazo kusanywa zitatumika kulipia shughuli za upandaji misitu kwenye halmashauri.

“Wazo hapa ni kupunguza ukataji holela wa misitu,” Ntalikwa alisema. Hata hivyo, Kuweka tozo hiyo huenda ikawa na mchakato mrefu kwa kuwa inahusisha mamlaka mbalimbali, alisema.

Chini ya mpango huo kila auzae mkaa ndani ya wilaya au anasafirisha nishati hiyo kutoka huko atalipa kodi ya shilingi 30,000 kwenye kila mfuko wa kilo 90.

Kodi hiyo ambayo ni lazima ithibitishwe na bunge, italipwa kwenye vituo maalum vya ukaguzi vitakavyowekwa kwenye kila wilaya.

Nchini Tanzania zaidi ya ekari 370,000 za misitu huharibiwa kila mwaka, kiwango kikubwa kwa matumizi ya nishati, kwa mujibu wa Wakala wa Misitu yenye mamlaka ya kuangalia matumizi mbalimbali ya misitu.

Jumanne Maghembe, waziri wa Maliasili na Utalii alisema mwezi December kwamba ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa ni lazima uachwe kwa kuwa unasababisha jangwa.

“Nadhani tukiweka tozo kubwa kwenye mkaa bei yake itapanda maradufu and watu wachache watashawishika kukata mitu kwa ajili ya kuuza mkaa. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeokoa misitu yetu,” alisema.

 

 MBADALA?

Kwa mujibu wa Maghembe, kama serikali ikiufanya mkaa ghali mno itaendeleza kwa haraka matumizi ya nishati mbadala, kama vile gesi ya kupikia majumbani.

Kwa sasa, “hata kwenye maeneo yenye nishati mbadala watu wangali wanatumia mkaa, ni lazima tuwakatishe tamaa” alisema.

Mpango wa serikali, hatahivyo, utaathiri maelfu ya watumiaji wa mkaa kama chanzo chao kikuu cha nishati ya kupikia au wanaojipatia kipato kwa kuuza mkaa.

“Kama serikali haitaki watu watumie mkaa, nini zaidi watumie kwa kupikia?” Alisema Tatu Mkendo, muuzaji wa mkaa jijini Dar es Salaam mwenye umri wa miaka 28.

“Nadhani watu wengi sana wataathirika kama kweli wanataka tuache kutumia mkaa. Aibu!” Alisema, huku akikusanya vipande vya mkaa na mikono yake iliyochafuka akiweka kwenye mifuko midogo ya plastiki kwa ajili ya kuuza.

Mkendo aliyekaa kwenye kibanda kidogo cha mbao alisema hajawahi kufikiri kuacha kuuza mkaa lakini huenda akafanya hivyo kama mkaa utakuwa hauna faida.

Tani million mbili za mkaa zinatumika Tanzania kila mwaka, zaidi ya nusu ikiwa ni jijini Dar es Salaam, Serikali imesema.

Biashara ya mkaa inazalisha dola za kimarekani 650 million kwa mwaka, inatoa ajira kwa maelfu ya watu kama wazalishaji, wasafirishaji na wauzaji wadogo wadogo wa majiko ya mkaa, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Kaya nyingi maskini nchini Tanzania wanategemea misitu kama chanzo cha nishati, wakivuna misitu kutengeneza mkaa na kuuza mbao.

“Sidhani kama ni sawa kuzuia biashara ambayo inategemewa na watu wengi kwa kupata kipato. Tungalifundishwa kuzalisha mkaa bila ya kuathiri mazingira,” Alisema Milton Malembeka, mzalishaji wa mkaa wilaya ya Bagamoyo kaskazini mwa Bagamoyo.

 

MARUFUKU ZILIZOSHINDWA.

Serikali ilijaribu siku za nyuma kuzuia biashara ya mkaa, na hivi karibuni Mwezi July, ambapo mkuu wa mkoa wa shinyanga alizuia bila mafanikia biashara hiyo, akiilaumu kuwa ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.

Jitihada hizo zilishindwa, hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa jitihada ya kuongeza matumizi ya nishati mbadala kama vile gesi ya majimaji ya kupikia na umeme.

Baadhi ya watumiaji wanalalamika gesi hizo huenda zikawa ghali kuliko mkaa.

“Huwezi kuzuia kitu ambacho kimsingi ni nishati pekee iliyopo kwa kupikia mijini bila ya kuonyesha njia mbadala,” alisema Amelia Bulayo, Mtafiti katika idara ya ikolojia ya chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Licha ya kuwa Tanzania ina vyanzo mbalimbali vya nishati kama vile gesi asilia na jua, mkaa na kuni zinachangia kwa asilimia 85 ya matumizi ya nishati ya kupikia kwa mujibu wa Sera ya taifa ya nishati ya 2015.

Matumizi ya mkaa, hasa mijini yameongezeka maradufu miongo miwili iliyopita kutokana na kasi ya ukuaji wa miji na upungufu wa mbadala, sera inasema.

Matumizi hayo yanatarajiwa kuongezeka tena mpaka kufikia mwaka 2030 kutoka tani million 2.3 kwa mwaka, sera inasema.

Msukumo wa serikali kwa miongo miwili kutumia gesi asilia kwa kupikia yamefanikiwa kidogo, huku matumizi yakikua kutoka tani za metriki 24,000 mwaka 2011 mpaka tani 69,000 mwaka 2015, takwimu za serikali zinaonyesha.

Baadhi ya wakaazi wa Dar es Salaam wamesema kubadili matumizi ya mkaa yamepunguza gharama zao za kupikia.

Peter Muthamia amesema mtungi mdogo wa kilo 8 wa gesi anatumia kwa miezi miwili kwa gharama ya shilingi 18,000. Mkaa hugharimu karibu shilingi 30,000 kwa mwezi.

“Fanyeni gesi iwafikie watanzania wote” alisisitiza.

(Imeandikwa na Kizito Makoye;uhariri na Jo Griffin na Laurie Goering:; Tafadhali tambua Thomson Reuters Foundation, tawi la hisani na Thomson Reuters , inayoandika habari za majanga, mabadiliko ya tabia nchi, ustahimilivu, haki za wanawake na biashara haramu ya binadamu.Tembelea  news.trust.org/climate)

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->