Mavuno ya ngano yashuka Kenya, wakulima warejelea maharagwe

Thursday, 25 April 2013 10:10 GMT

Quick-to-grow crop produces a more reliable harvest as climate change brings erratic weather

Na Kagondu Njagi

NAROK, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Kwa miaka mingi, ilikuwa ni ngano iliyoletea familia ya Joshua Nyaruri mapato na lishe. Lakini hivi karibuni inaonekana mmea huu maarufu huko Bonde la Ufa washindwa na zao lililodharauliwa - maharagwe.

Kwa miaka sitini aliyoishi katika kijiji cha Ole Leshua huko kaunti ya Narok, Nyaruri anaunga wito unaosifu ngano kama moja ya mmea wenye thamani zaidi nchini Kenya.

Lakini zaidi ya muongo mmoja uliopita au zaidi, nafaka imekuwa ikishuka kutoka wito huu, kwa sababu ya hali ya hewa isiyotabirika, ambayo wataalam wanaamini inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Wakati tunatarajia mvua, msimu wa kiangazi unaendelea,” asema baba huyu wa watoto watano. “Wakati tunahitaji jua ili mazao iive, mvua inayoendelea inahakikisha nafaka iliyobaki inaoza mashambani.”

Badala yake, wakulima wanaamua kulima mazao mapya ambayo yanaweza kuhimili shinikizo za mabadiliko ya hali ya hewa, wadudu na magonjwa, Nyaruri asema, na kuzidi kuhisi kuwa kilimo cha ngano ni sawia na kupoteza bidii.

SHINIKIZO KWA NGANO

Safari kupitia barabara sugu ambayo inapitia eneo lililo na vipande vikubwa vya ardhi ya kilimo huku Bonde la Ufa, kuna mashamba machache yanayoonekana kuchipua ngano kiwango cha goti. Chache zina masuke ya ngano.

Kawaida, “wakati huu wa mwaka, mimea mingi ingekuwa imetoa kokwa,” aelezea Charles Ngare, mkulima ambaye amekuwa akilima ngano karibu miongo mitatu. “Nadhani ukomavu huu wa polepole ni kwa sababu mvua ilichelewa.”

Lakini katika shamba la Nyaruri, lililo umbali wa kama kilomita kumi, mkulima huyu anapuria mavuno yake ya hivi karibuni ya maharagwe. Yeye aliachana na kilimo cha ngano miaka mitano iliyopita na hana majuto kwa uamuzi wa kubadilisha, aelezea.

“Mimi nilipanda maharagwe katikati ya mwezi wa Desemba mwaka jana na mapema Machi nilikuwa nikivuna,” ahimili Nyaruri, akielekeza kichwa kwa sehemu ya shamba ambayo imelimwa upya ili kuiandaa kwa ajili ya msimu ufwatao wa kupanda.

Kado na sehemu iliyopaliliwa, sehemu lingine lina safu za maharagwe mbichi inayoning’inika na zao. Haya maharagwe yatakuwa tayari kuvunua baada ya wiki sita, yeye awaza.   

Anapoonyesha shamba lake la hekari sabini, yeye ajisifu kwa vile vuno lake limekuwa likinawiri akilinganisha na wakati alipokuwa akilima ngano.

Mkulima huyu asema kwamba kilo mbili za mbegu ya maharagwe ndizo zilizalisha kilo sitini na tano, na kuwa zilichukua miezi mbili na nusu tu kukomaa.

Kama angelikuwa amepanda ngano mwezi wa Desemba, asema, bado angekuwa akisubiri vuno la kwanza. Kwa kawaida, ngano hukomaa baada ya miezi minne na inahitaji mvua zaidi ya milimita mia nane na sitini kwa mwaka.

Wanyama pori na ndege za kuhama hama pia hutishia ngano. Lakini aina hii mpya ya maharagwe haipendwi na wanyamapori, kulingana na watafiti.

Maharagwe haya katika shamba la Nyaruri yaliundwa na taasisi ya utafiti ya kilimo ya Kenya, (KARI) Katumani, ikishirikiana na shirika la maendeleo ya sayansi Afrika mashariki, (Bio – Innovate), na washirika wengine.

MAHARAGWE INAYOKOMAA HARAKA

Maharagwe hii hukomaa haraka, huhitaji mvua kidogo kukua, na hata huchukuliwa kutumia nishati kidogo kwa sababu hupikika haraka ikilinganishwa na maharagwe ya jadi, kwa mujibu wa wanasayansi wa KARI.

Vumbuzi hizi zavutia idadi kubwa ya wakulima nchini Kenya, na katika nchi zingine zilizo na hamu ya kukabiliana na changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

David Karanja, mratibu wa mradi wa jamii ya kunde ya kijani kibichi huko KARI - Katumani, aelezea kuwa aina hii mpya huchukua siku thelathini baada ya kuota maua, na zingine thelathini na tano zikuwe tayari kuvuna.

Zile za jadi huchukua siku tisini kutoa maua na zingine thelathini kuwa tayari kuvuna.

Pia la muhimu, “aina hii mpya yaweza kuwa na mavuno zaidi ya mara mbili kwa kila ekari moja ikilinganishwa na maharagwe ya jadi,” asema Karanja.

MEZANI

Maharagwe haya pia hupikika kwa kasi na yana lishe tamu, mambo ambayo ni vutio kwa watu kama Beatrice Kirui, ambaye ameyaorodhesha kama ongezeko la mlo kwa familia yake.

Mama huyu wa umri wa miaka ishirini na sita apea mtoto wake wa miezi nne uji wa maharagwe haya wakati akimbembeleza hapo nje ya duka lake huko kijiji cha Olereut.

 “Mimi husiaga maharagwe haya ili kutengeneza uji,” asema mama huyu wa watoto wanne. “Ninatumia kuni chache kwa sababu maharagwe haya yanaiva kwa haraka ikilinganishwa na yale ya jadi.”

“Watoto wanayapenda pia kwa sababu hayaleti gesi katika tumbo,” aongeza.

Katika kijiji chake, kama kilomita themanini kutoka shamba la Nyaruri, mahindi, maharagwe na ngano ndio vyakula vikuu toka enzi za jadi.

Kirui asema kupungua kwa mavuno kwa mazao yote matatu inatokana na hali ya hewa isiyo ya uhakika na magonjwa, pengine inayohusishwa na mabadiliko ya joto na mabadiliko ya hali ya hewa.

Miaka mitatu iliyopita, magonjwa ya ajabu yamemekuwa yakiathiri mimea, asema. Haya ni pamoja na shina kutu ya ngano, ambayo wataalam watuhumia ililetwa Kenya na barugumu la upepo kutoka nchi ya Ethiopia.

Utafiti wa shirika la umoja wa mataifa, FAO, nao waonyesha kwamba pato la ngano Kenya limekuwa likishuka tangu mwaka wa elfu moja mia tisa na sabini.

Lakini Dan Sirari, anayefanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali la CLUSA Kenya na ambalo latetea maendeleo ya ushirika miongoni mwa wakulima wadogo wadogo, atumai kwamba mimea mipya itaweza kujenga usalama wa chakula kwa wakulima wanaojitahidi sana.

 “Mbinu hizi za kilimo zinawapa wakulima fursa kujaribia mazao bora na yanayofaa katika mashamba yao,” asema.

Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira mjini Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.